Welcome to Cluster!

...
Kongano La Nguo Morogoro (kongumo)

2.1.KONGANO LA NGUO MOROGORO (KONGUMO) ni asasi ya kijamii ilioanzishwa kwa lengo la KUWAUNGANISHA MAFUNDI NGUO MMOJA MMOJA NA WADAU WA SEKTA YA NGUO ili:-  Kuinua kiwango cha Ubunifu na Utengenezaji wa Nguo zitakazoweza kushindana katika Soko huria ambalo linajumuisha bidhaa za nguo kutoka nje ya Tanzania.  Kuongeza na kujenga ujuzi wa ushonaji na kiwango cha uzalishaji katika kiwango kinachokubalika kwa wavaaji ili kumiliki soko la ndani.  Kutengeneza nguo bora na kusambaza katika mikoa mbali mbali.  Kushiriki katika Uanzishajishaji wa Kiwanda cha Nguo kitakachomilikiwa na wanachama.  Kuongeza ajira kwa vijana hususani wale wote wanaomaliza masomo katika shule za msingi na sekondari ambao hawatapata nafasi za kuendelea na mfumo wa elimu Rasmi.  Mwisho ni kuinua kiwango cha Ubora wa maisha kwa Mafundi waliopo Morogoro na sehemu nyingie Tanzania ikiwa ni njia ya kupigana vita na Umasikini wa kipato. Kikundi kimesajiliwa kisheria na kupewa hati ya usajili namba MG/MMC/CBO/01010 ya tarehe 11/04/2016. Shughuli kuu za kikundi ni kuwaunganisha wanachama MAFUNDI NGUO, WADAU WA SEKTA YA NGUO na wasio wanachama katika ushiriki wa Uzalishaji na uendeshaji wa Sekta ya Nguo. Pamoja na kuwa Sekta ya nguo ndio Muhimili wa kikundi Pia KONGUMO inajishughulisha na Miradi mbali mbali ya uzalishaji mali ikwemo shughuli za kilimo pia ni wafugaji wa aina mbali mbali za ufugaji. Eneo la kipaumbele. Kuanzisha Viwanda Vidogo kushiriki katika Uchumi wa Viwanda Kwa Lengo la Kuongeza Ajira Na kuinua Uchumi kwa Kikundi na wanachama wa KONGUMO. Pamoja na nia njema ya ushiriki katika uchumi wa viwanda hususa ni katika sekta ya nguo KONGUMO na wanchama wake wanakabiliwa na changamoto zifuatazo

About

Kongano hili linaitwa Kongano la Nguo Morogoro (KONGUMO) na lilianzishwa tarehe 12 -03- 2013 . Lengo kuu lilikuwa kutambuana /kufahamiana, kutengeneza umoja wa kufanya kazi kwa pamoja ili kubadilishana ujuzi na uzoefu na kuwa na sauti moja. Kongano hili lina wanachama 51 (Hamsini na moja) wote wakiwa wazalishaji.

Goals

" Kuwa bora katika ubunifu, utengenezaji wa nguo na bidhaa zake na kutosheleza soko la ndani ya nchi na nje"

Mission

"Kuwa na umoja wa mafundi walioungana kwa Nguvu za pamoja kufanya kazi kwa bidii na kujenga ujuzi, ufahamu na weledi ili kutosheleza mahitaji ya nguo na bidhaa zake Tanzania"

Objectives

   (i) Kujengea uwezo wanachama  ufahamu wa njia sahihi za uendeshaji na ukuzaji      nguo wa biashara ili kupunguza utegemezi wa bidhaa toka nje.

(ii)Kutoa ushauri/utaalamu  kwa wanachama juu ya Ubunifu na ushonaji wa nguo kwa kiwango bora.

(iii)Kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Miundombinu mbali mbali itakayochochea uzalishaji wa nguo na bidhaa zake  kwa kutumia wataalamu kwa mfumo shirikishi jamii.

(iv).Kutafuta MASOKO ya Bidhaa za nguo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi.

(v). Kupanga Kuanzisha kusimamia viwanda Vidogo vidogo vya ushonaji kwa njia ya ushirikiano.

(vi) Kuwajengea uwezo wa kubuni ,kuendesha na kusimamia miradi mbali mbali ya kiuchumi katika sekta ya mbali mbali za kiuchumi  kilimo,ufugaji na biashara pamoja na mbinu za utafutaji wa masoko kwa ushirikiano na wataalamu wa sekta husika.

(vii) Kutoa elimu Kwa wanachama na jamii kama vile sera mbalimbali za taifa zenye athari katika maisha ya kila siku ya mwananchi.

 

(viii).Kuwajengea uwezo wanachama na jamii elimu ya utawala bora na maadili katika utumishi wa umma ili kufahamu haki na wajibu wao katika Taifa.

 

(ix).Kuelimisha jamii juu ya elimu ya vvu/ukimwi pamoja na uwezeshaji kwa watu ambao ni wathirika wakiwemo yatima wajane na wazee.

 

 (x).Ushawishi ushirikishaji wa jamii katika kujiunga katika vikundi vya uzalishaji kwa faida, uwekaji na ukopeshaji wa fedha, ushirika wa uzalishaji.

 

(xi). Kushirikiana na wadau wa maendeleo katika jamii katika kutoa huduma zinazolenga ustawi wa jamii.

Challenges

i.  KIWANGO KIDOGO/HAFIFU CHA MTAJI WA KUSHIRIKI KATIKA UANZISHAJI WA KIWANDA CHA NGUO.             

ii.   ENEO LA KUTOSHA KWA AJILI YA KUJENGA KIWANDA KITAKACHOWEZESHA KUFUNGA MASHINE TOSHELEZI KATIKA MFUMO WA VIWANDA VYA NGUO.

iii. MASHINE ZA KISASA ZINAZOENDANA NA UZALISHAJI WA NGUO BORA ZINAZOWEZA KUSHINDANA KATIKA SOKO.

iv. MALI GHAFI KATIKA UZALISHAJI (MTAJI MDOGO).

KONGUMO's News

Contact Us

Name Kongano La Nguo Morogoro (kongumo)
Email kongumo26@gmail.com
Phone number 0655893307/0784 435 383/0757 326 869
Address Morogoro
Location P.O.BOX 6824
Region Morogoro
District Morogoro Mjini
Ward Mji Mkuu

Our Products

mashati vitenge na Rangi moja Cotton 100%
mashati vitenge na Rangi moja Cotton 100%
Magauni KitengeRangi Moja

Firms

# Name Activity
1 Mama Halima Africa Fashion Ushonaji wa Nguo aina zote za kike na kiume
2 Eveta Tailoring Kutengeneza rasilimali watu na utengenezaji wa Batiki
3 Kapunguti Tailoring Ushonaji wa nguo za kike na kiume
4 Eddy Fashion Ushonaji wa Nguo za kike na kiume pamoja na Kudarizi
5 Graceline Fashion Ushonaji wa Nguo za kike na kiume pamoja na kudarizi
6 Mkwawa Fashion Kutengeneza rasilimali watu na kushona Nguo aina zote za kike na kiume
7 Galilaya Tailoring Roberth Mathias Ushonaji wa Nguo aina zote za kiume na kike
8 Akapagala Designer Ushonaji wa Nguo aina zote za kike na kiume
9 Emgo Tailoring Utengenezaji wa Begi na Begi za mkononi na Nguo aina zote
10 Geness Tailoring Ushonaji wa Nguo aina zote zakike na kiume
11 Elishadai Ushonaji wa nguo aina zote za kiume na za kike
12 Stahima Tailoring Mat Ushonaji wa Nguo aina zote za kike na kiume
13 Belina Tailoring Ushonaji wa Nguo aina zote za kike na kikume
14 NEW JERICHO FASHION & DESIGNER KUSHONA NA KUUZA NGUO ZA KIAFRIKA
15 KIPEJA TAILORING MART KUSHONA NGUO ZA AINA ZOTE ZA KIKE, KIUME NA WATOTO