- Kiwango Leather Cluster
- Thu, Jun 2, 2022 7:00 PM
Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mh. Joseph Tadayo atembelea banda la Kongano la Ngozi LA KIWANGO katika maonyesho ya ubunifu 2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Mheshimiwa amejionea na ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na kongano na kutambua mchango wa kongano katikakutengeneza ajira. Pia mheshimiwa ameipongeza na kuishukuru COSTECH kwa juhudi zao za kuibua na kuwezesha kongano bunifu Tanzania hasa kwa kuwauganisha na taasisi za maarifa ambazo zimeongeza tija katika ubora wa bidhaa na kutatua changamoto za kongano. Mheshimiwa ameahidi kutembelea kongano ili kujionea fursa zilizopo ili kuweka mkakati kwa Jamie ya mwanga kunufaika kiuchumi kupitia shughuli za kongano.